Mkutano huo unafanyika siku chache kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP30 utakaonza wiki ijayo.

Miongoni mwa viongozi watakaohuduria ni Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Katika mkutano huo karibu kila taifa litashiriki japo Marekani haitakuwa na mwakilishi yoyote.

Juhudi zaidi zatakiwa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi

Viongozi wa dunia wameendelea kulaumiwa kwa kusuasua katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Mapema Jumatano, wanaharakati wa mashirika kadhaa walifanya maandamano katika mji wa Belem kunakofanyika mkutano huo wakishinikiza hatua zaidi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *