Juhudi hizo zinafanyika wakati ambapo Rais wa Marekani Donald Trump anajaribu kuushinikiza Umoja wa Ulaya ununue gesi kutoka Marekani. Mkutano huo unafanyika wakati Urusi na Ukraine zikiendelea kupambana. Jeshi la Ukraine limesema limeulenga mtambo wa kusafisha mafuta wa Volgograd wa Urusi na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Mmoja auwawa kwa mashambulizi ya droni Urusi

Gavana Andrei Bocharov amesema mtu huyo ameuawa kwa kuangukiwa na mabaki ya droni yaliyosababisha moto mkubwa katika eneo la viwanda wakati vikosi vya Urusi  vinaendelea kusonga mbele Kaskazini mwa Pokrovsk nchini Ukraine kwa lengo la kuudhibiti kikamilifu mji huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *