
Waangalizi hao wamebainisha kuwa uchaguzi huo haukuzingatia pia kanuni za Umoja wa Afrika na viwango vingine vya kimataifa vya uchaguzi wa kidemokrasia.
Aidha wametaja kuwepo kwa matukio ya udanganyifu ikiwemo kujazwa kura zisizo halali ndani ya masanduku katika vituo kadhaa vya kupigia kura. Vilivile ripoti hiyo imesema waangalizi wake walishuhudia watu wakipewa karatasi nyingi za kupigia kura na wengine waliruhusiwa kupiga kura bila kuonesha vitambulisho.
Maandamano, vurugu vyatajwa katika ripoti ya waangalizi
Ripoti ya waangalizi hao imeeleza pia juu ya kuwepo kwa maandamano ya vurugu, milio ya risasi, kufungwa kwa barabara, na kuchomwa kwa matairi katika baadhi ya mikoa ikiwemo Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Kagera, Dodoma, Kigoma, Tabora, Buhungwa, Singinda. Umoja wa Afrika umeitaka Tanzania kuyapa kipaumbele mageuzi ya sheria za uchaguzi na kisiasa ili kushughulikia sababu kuu za changamoto zake za kidemokrasia na uchaguzi.