Kundi la Hamas liliurejesha mwili wa Mollel Jumatano jioni kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyoratibiwa na Marekani. Katika tukio jingine, Jeshi la Israel limethibitisha kuwa limewauwa Wapalestina wawili katika Ukanda wa Gaza likiwatuhumu kwa kulikaribia kwa vitisho eneo lililo chini ya udhibiti wake.

Mpalestina mwingine auawa akitafuta kuni

Mamlaka za Afya za Gaza zimesema mashambulizi ya Israel yalimuua pia Mpalestina mwingine aliyekuwa akikusanya kuni katikati mwa ukanda wa Gaza. Israel hata hivyo imesema haifahamu lolote kuhusu mauaji ya mtu huyo kwenye eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *