Israel imesema kuwa kikundi cha Hamas kimerejesha mabaki ya aliyekuwa mwanafunzi wa Kitanzania, Joshua Loitu Mollel.

Mollel ambaye alikuwa anasomea kilimo nchini Israel, alichukuliwa kinguvu na kuuwawa wakati wa shambulio la Oktoba 7 katika eneo Kibbutz Nahal Oz.

Kikundi cha Hamas kinadaiwa kurudisha mwili wa Mollel siku ya Jumatano Novemba 5, 2025 ikiwa ni baada ya siku 761, kama sehemu ya mpango wa usitishwaji vita vya Gaza, ambao uliratibiwa na Rais Donald Trump wa Marekani.

“Baada ya kukamilika kwa shughuli ya utambuzi… wizara ya mambo ya nje imeijulisha familia ya mateka huyo kuwa mwili wa mpendwa wao umerejeshwa,” Ofisi ya Waziri Mkuu ilisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *