Majaji wa mahakama hiyo wamesema kuna sababu za kutosha kuwa Kony alihusika na mashtaka 29 kama mhusika asiye wa moja kwa moja.

Makosa yanayohusishwa na Kony

Haya yanahusiana na mashambulizi yaliofanywa na kundi la waasi wa Lord’s Resistance Army, LRA,  dhidi ya shule na kambi za wakimbizi wa ndani ikiwa ni pamoja na mauaji, mateso, ndoa za lazima, mimba za kulazimishwa, ubakaji, na kuwasajili jeshini watoto walio na umri wa chini ya miaka 15.

Mahakama hiyo ya ICC pia imesema Kony alikuwa na kesi ya kujibu kama mhusika wa moja kwa moja katika kesi 10 zinazohusiana na waathiriwa wawili waliolazimishwa kuwa wake zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *