Katika taarifa ya pamoja na mashirika mengine sita yasiyo ya kiserikali, Kituo cha Sheria na Haki za Kibinadamu (LHRC) kimesema kulikuwa na “matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wasio na silaha.

LHRC pia imesema familia zimeachwa zikiwa na kiwewe, na watoto wameshuhudia ukatili dhidi ya wazazi wao.

Vijana ndio waliolengwa katika ghasia nchini Tanzania

Taarifa hiyo imeendelea kusema vijana hasa ndio waliokuwa walengwa na kwamba mamia ya watu wamekamatwa, wengine wakisalia kizuizini bila dhamana.

Imeonya kuwa kiwango cha ukiukwaji wa haki za binadamu bado hakijafichuliwa kikamilifu, ikikosoa kukatizwa kwa mtandao na vikwazo dhidi ya vyombo vya habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *