
Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imesema raia wa Urusi watalazimika kuomba viza mpya kila wanapotaka kuingia Ulaya kwa lengo la kuwachunguza mara kwa mara waombaji wa viza hizo ili kupunguza uwezekano wa hatari.
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wajenga mazingira hatari
Katika taarifa, mjumbe maalumu wa Umoja huo Kaja Kallas, amesema kwa miongo kadhaa, uvamizi haramu wa Urusi dhidi ya Ukraine umejenga mazingira hatari zaidi ya usalama Ulaya.
Pia amesema kwa sasa wanakabiliwa na usumbufu wa droni na hujuma kwenye ardhi yao kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Kallas pia amesema ni jukumu la Umoja huo wa Ulaya kuwalinda raia wao.