
Rais wa Marekani Donald Trump alisema Ijumaa kuwa hakuna afisa wa Marekani atakayehudhuria mkutano wa G20 nchini Afrika Kusini, akiishutumu nchi hiyo kwa “ukiukaji wa haki za binadamu” dhidi ya wakazi wa Afrikaner.
Katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump aliikosoa Afrika Kusini kwa “mauaji na uchinjaji” wa Waafrikana na “kunyang’anywa” mashamba na ardhi yao kinyume cha sheria.
Waafrika ni vizazi vya walowezi wa Uholanzi, Wafaransa na Wajerumani huko Afrika Kusini. “Ni aibu kubwa kwamba G20 itafanyika Afrika Kusini,” Trump aliandika. “Wa Afrikan wanauawa na kuchinjwa, na ardhi na mashamba yao yanatwaliwa kinyume cha sheria. Hakuna Afisa wa Serikali ya Marekani atakayehudhuria maadamu ukiukaji huu wa Haki za Kibinadamu unaendelea.”