Hapo jana, Kibatala aliiambia AFP kwamba mamia ya watu walifikishwa mahakamani jijini Dar es Salaam.

Idadi ya watu 250 waliowajumuisha wake kwa waume, walishtakiwa kwa kesi tatu tofauti na wote kukabiliwa na mashtaka mawili tofauti.

Shtaka la kwanza ni njama ya kufanya uhaini na la pili ni uhaini wenyewe.

Baadhi ya viongozi wa upinzani Tanzania wasakwa na polisi

Huku hayo yakijiri, msemaji wa jeshi la polisi Tanzania David Misime amesema jana kuwa wanawasaka  viongozi wa vyama vya upinzani akiwemo katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika, naibu wake Amani Golugwa, na msemaji Brenda Rupia kuhusiana na vurugu hizo za uchaguzi.

Katika taarifa, Misime amewataka watu huo kujisalimisha kwa polisi mara moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *