Naibu Katibu Mkuu Bara wa CHADEMA Amani Golugwa amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha Jumamosi asubuhi.

Taarifa ya kukamatwa kwake imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia ambaye pia ametajwa katika orodha ya wanasiasa wa upinzani wanaosakwa na polisi Tanzania kwa madai ya kuchochea maandamano yaliyoishia kwa ghasia na vifo.

‘‘Kukamatwa kwa Naibu katibu Mkuu kunaamisha kwamba serikali imewaacha nje viongozi watatu tu kati ya sita wa chama,’’ ilisema taarifa ya CHADEMA iliyochapishwa mtandaoni.

Mamlaka ya Tanzania iliwashtaki mamia ya watu kwa kosa la uhaini kutokana na maandamano hayo katika uchaguzi uliozozaniwa mwezi uliopita, katika hali iliyozidisha mvutano wa kisiasa.

Mbali na makumi ya mashitaka ya jinai siku moja mapema jijini Dar es Salaam, makumi ya wengine wanakabiliwa na mashtaka kama hayo ya uhaini mahali pengine katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kulingana na rekosi za mahakama ambazo zilipatikana hadharani Jumamosi.

‘‘Tunaelewa kuwa serikali ina mpango wa kuwakamata na kuwapa kesi ya uhaini viongozi wetu ili chama kikose viongozi wa kukiendesha na kipoteze uelekeo,’’ alisema Naibu Katibu Mkuu Brenda Rupia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *