Huduma za uokoaji zimesema moto ulizuka katika jengo hilo na vyumba kadhaa kuharibiwa. Maafisa wa uokoaji walipata miili ya watu hao watatu huku watoto wawili wakiwa miongoni mwa waliojeruhiwa.

Shambulizi hilo katika eneo hilo la Dnipro, mji wa nne kwa ukubwa nchini Ukraine, lilikuwa sehemu ya shambulizi kubwa la kombora na droni la Urusi kote nchini humo, lililolenga miundombinu ya nishati na pia kuuwa mfanyakazi mmoja katika kampuni ya nishati huko Kharkiv. Haya ni kwa mujibu wa afisa mmoja katika eneo hilo.

Katika upande wa mashariki mwa Ukraine, mapigano kwa ajili ya mji wa kimkakati wa Pokrovsk yamefikia hatua muhimu, huku Kyiv na Moscow zikishindana kumdhihirishia rais wa Marekani Donald Trump kwamba wanaweza kushinda kwenye uwanja wa vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *