Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, ofisi hiyo ya ODPP imesema hatua hiyo ni matokeo ya juhudi kubwa zilizoratibiwa kati ya mamlaka za Kenya na Uingereza.

Pia imesema kuwa ODPP inasisitiza dhamira yake isiyoyumba ya kutafuta haki kwa Wanjiru na familia yake, kwa ushirikiano na washirika wa kimataifa, ili kuhakikisha kwamba waliohusika wanawajibishwa kikamilifu.

Kesi ashtumiwa kwa kumuua Wanjiru mwaka 2012

Wakati huo huo kupitia taarifa, Shirika la Kitaifa la Uhalifu la Uingereza, limesema Purkiss mwenye umri wa miaka 38, aliwekwa rumande na hakimu baada ya kukamatwa siku ya Alhamisi.

Purkiss amekuwa akisakwa nchini Kenya kwa tuhuma za kumuua Wanjiru aliyekuwa na umri wa miaka 21 mnamo mnamo mwaka 2012 katika kesi ambayo imesababisha mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *