Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amevipongeza vikosi vya usalama vya nchi hiyo kwa kuvunja mtandao wa ujasusi uliounganishwa na mashirika ya ujasusi ya Marekani, Israel na Saudi Arabia, akisema kuwa kundi hilo la ujasusi lilitaka zaidi kupunguza uungaji mkono na himaya ya serikali ya Sana’a kwa Palestina.

Katika taarifa yake ya leo Jumapili, Mahdi al-Mashat amesema, mafanikio ya usalama yanaonyesha kiwango cha uadui na uchokozi wa Marekani, Israel na Saudi Arabia dhidi ya Yemen.

“Hii inakuja huku kukiwa na mashambulizi na hatua zinazoongezeka ambazo zinalenga kudhoofisha au kusimamisha himaya na uungaji mkono wa Yemen kwa ndugu na dada zetu huko Gaza, mapambano yao na haki halali za taifa la Palestina,” amesema Mahdi al-Mashat.

Amepongeza ushirikiano, umakini na uelewa wa matabaka yote ya jamii ya Yemen, akisisitiza kwamba njama zote za maadui zimeshindwa mbele ya ustahimilivu na kusimama imara kwa taifa hilo.

Mashat amehusisha mafanikio makubwa yaliyopatikana na mafundisho ya Qur’ani, akisema yamechangia pakubwa katika kuelewa asili ya mapambano dhidi ya maadui wa taifa la Yemen – hasa Marekani na Israel – na jinsi ya kukabiliana nao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *