Mkutano huo uliofanyika kwenye mji wa pwani ya Kolombia, Santa Maria, kati ya Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Mataifa ya Amerika Kusini na Karibi, ulidhamiria kuanzisha uratibu wa pamoja kati ya mamlaka za polisi, mahakama, na forodha za pande hizo.

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, alisema ushirikiano wao utafanya mengi zaidi ya kuwalinda raia, ambapo mpango wa Umoja wa Ulaya kulinda njia za baharini utatanuliwa kuwezesha upashanaji habari na uchukuwaji hatua za pamoja dhidi ya uhalifu baharini.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Rais Lula da Silva wa Brazil, Rais wa Baraza la Ulasa, Antonio Costa na Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *