Vyombo vya habari nchini Marekani, vikiwemo vituo vya CNN na Fox News, viliripoti kwamba watunga sheria hao wameafikiana kuruhusu ufadhili kwa serikali kuu hadi mwezi Januari baada ya kubishana sana juu ya ruzuku kwenye huduma za afya, mafao ya chakula na hatua ya Rais Donald Trump kuwafuta kazi wafanyakazi kadhaa wa serikali kuu.

Makubaliano hayo yalitazamiwa kupigiwa kura na Bazara la Seneti usiku wa Jumapili. 

Hata hivyo, makubaliano hayo yamefikiwa baada ya hasara kubwa sana, hasa kwenye sekta ya usafirishaji, ambapo zaidi ya safari 7,000 zilicheleweshwa siku ya Jumapili (Novemba 9), huku zaidi ya 1,000 zikifutwa siku ya Ijumaa, na zaidi ya 1,500 siku ya Jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *