Halmashauri ya Jiji la Tanga imeanza kutekeleza mradi wa kufunga kamera za ulinzi na taa za barabarani kwa lengo la kuboresha usalama na mandhari ya mji huo.
Kupitia mradi huo unaotekelezwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, jumla ya taa 600 na kamera 120 zinatarajiwa kufungwa, huku utekelezaji wake ukiwa umefikia asilimia 28 hadi sasa.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi