
DAR ES SALAAM: CHAMA cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) kimelaani vurugu na uharibifu wa mali uliotokea Oktoba 29 siku ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Chama hicho pia kimetoa pole kwa waliopoteza ndugu au mali, hata hivyo TPBA imeunga mkono agizo la Rais Dk Samia Suluhu Hassan la kufanya uchunguzi wa kina na kuwawajibisha wahusika wote kwa mujibu wa sheria.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Katiba ya 1977 inatambua haki za binadamu kama uhuru wa maoni na maandamano, lakini haki hizo zina mipaka ya kisheria kulinda amani na usalama wa taifa.
“Maandamano ya tarehe 29 Oktoba 2025 hayakuwa halali, kwani yalikiuka zuio la polisi na kusababisha vurugu,”
“TPBA inasisitiza kuwa matumizi ya nguvu na silaha yanapaswa kuwa ya kiwango cha lazima pekee na kwa uwajibikaji wa kisheria. Kuhusu changamoto za intaneti, mamlaka zinaweza kudhibiti mawasiliano kwa muda kwa mujibu wa sheria kulinda usalama wa taifa,”ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.