#HABARI: Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Bwana Tundu Lissu ameibua hoja sita nzito mbele ya jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo ya Uhaini baada ya kupinga shahidi wa tatu kutoa ushahidi wake kwa kificho kwenye kizimba maalumu kwa ajili ya kumficha shahidi anayetoa ushahidi akidai utaratibu huo ni kinyume cha sheria ya ulinzi wa mashahidi.
Akitumia muda wa saa 3 na dakika 48, Lissu ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo ya uhaini na kutimiza siku 223 akiwa mahabusu Ukonga, amedai hata sheria inayotumia kuwaficha mashahidi haikuchapishwa katika gazeti la Serikali hivyo sheria hiyo kutokuwa na uhalali wa kutumika kwa kuwaficha mashahidi katika kesi zingine.
Kesi hiyo imeharishwa mpaka Msajili wa Mahakama atakapopanga kikao kingine cha mahamaka ambacho kitapanga kuendelea kwa mfululizo wa tarehe za kusikiliza kesi hiyo ambapo mawakili wa upande wa Jamhuri watajibu hoja zote sita ambazo zimeibuliwa na Lissu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.