Msemaji wa serikali ya Iran ameeleza kuwa Iran itatoa jibu kali zaidi na kwa nguvu kubwa” ikilinganishwa na wakati uliopita ikiwa itakabiliwa na na uchokozi mpya wa nchi ajinabi.

Bi Fatemeh Mojajerani ameeleza hayo jana katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya al- Mayadeen ya Lebanon na kusisitiza kuwa kuhusu azma ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kulinda mamlaka ya kujitawala ya nchi na watu wake. 

Akizungumzia vita visivyo na msingi vya Israel na Marekani dhidi ya Iran mwezi Juni mwaka huu, Msemaji wa serikali ameeleza kuwa Iran haitazingatia hisia za nje wakati wa kulinda na kuihami ardhi yake. 

Fatemeh Mohajerani pia amesisitiza kuhusu uwezo wa makombora wa Iran na kueleza kuwa huku Tehran sasa inashughulikia udhaifu uliojitokeza wakati wa mashambulizi hayo.

Ameongeza kuwa mwelekeo wa Iran hautegemei kauli mbiu, bali vitendo,” na kusisitiza kuwa Iran imejiandaa kimkakati kukabiliana na vitisho vyovyote dhidi yake. 

Msemaji wa serikali ya Iran ameendelea kusema, kwa upande wa diplomasia mazungumzo yanayoendelea ya nchi za Magharibi hayana maana iwapo anga ya mazungumzo hayo ni ya mashinikizo licha ya Iran kupokea jumbe zisizo za moja kwa moja kuhusu uwezekano wa kufanyika mazungumzo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *