Nchini Marekani mabunge yote yamekubaliana kuruhusu idara ya sheria kuweka wazi nyaraka kuhusu mshukiwa wa tuhma za ngono dhidi ya watoto, Marehemu Jeffrey Epstein.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Bunge la Wawakilishi limeidhinisha hatua hiyo kwa kura 427-1, huku bunge la Seneti likisema litapitisha mswada huo kabla ya kuupokea.

Rais Donald Trump amesema yupo tayari kusaini mswada huo, ili nyaraka hizo ziwekwe wazi, baada ya shinikizo kutoka kwa raia wa Marekani.

Hatua hii inakuja baada ya manusura wa Epstein kujitokeza na kuunga mkono hatua ya taarifa hizo kuwekwa wazi, baada ya kuteseka kwa muda mrefu.

Taarifa hizo zinatarajiwa kuonesha kuhusu uchunguzi uliofanyika, na mahojiano yaliyofanywa kutoka kwa waathiriwa.

Jeffrey Epstein, mchumi maarufu wa Marekani alipoteza maisha mwaka 2019, kwa kujinyonga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *