Jeshi la Urusi limetekeleza shambulio kubwa kwenye mji wa Magharibi wa Ternopil nchini Ukraine na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 20, wakiwemo watoto wawili.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mauaji haya yamekuja, wakati rais wa Ukraine Vlodymr Zelensky, akizuru Uturuki kuona uwekezekano wa kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya amani.
Mpaka Jumatano jioni, Wizara ya Mambo ya ndani ya Ukraine, imesema watu waliopoteza maisha ni 25, huku wengine zaidi ya 70 wakijeruhiwa, wakiwemo watoto 15.
Shambulio hili lilitokea siku ya Jumatano Alfajiri, ndilo baya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Ukraine, katika siku za hivi karibuni.

Aidha, Ukraine inasema wanajeshi wa Urusi, wamerusha makombora 48 na kutumia ndege zisizo na rubani zaidi ya 400 kwenye shambulio hilo.
Kabla ya kuelekea Uturuki, Zelensky aliyataka mataifa ya Magharibi, yakiongozwa na Marekani kufanya jitihada zaidi za kumaliza uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.