Watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya nchini Comoro wametembelea kwa wenzao wa TAKUKURU kwa lengo la kujifunza mbinu na mikakati ya kukabiliana na rushwa nchini kwao baada ya kuridhishwa na mwenendo ubora wa viwango vya Tanzania katika kudhibiti rushwa kimataifa.
Taasisi hiyo, NCPCC imeleta baadhi ya watendaji wake wakiongozwa na Rais wa mamlaka hiyo, Fahamoe Youssouf aliyesema uzoefu wa TAKUKURU na uwezo wake katika ukanda wa Afrika umewavutia kuja kujifunza.
Imeandaliwa na Esterbella Malisa
Mhariri @moseskwindi