
Ripoti hiyo imewekwenda mbali na kusema kuwa takriban wanawake na wasichana 83,000 dunianiwaliuawa kwa makusudi mwaka uliopita wa 2024, na asilimia 60 ya matukio hayo yalifanywa na wanafamilia au wapenzi wao. Umoja huo uliyasema hayo huku huku ukitoa ripoti yake ya kila mwaka juu ya siku ya Kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake.
Upande wa mauaji ya wanaume ni asilimia 11 ndio wanaouawa na watu wa familia na wapenzi wao, idadi inayoonekana kuwa ya chini ukilinganisha na mauaji ya wanawake.
Ripoti hiyo ambayo ni ya hivi karibuni inayoangazia mauaji ya wanawake au wasichana kwaajili tu ya jinsia yao, ilitolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya mihadarati na uhalifu (UNODC) pamoja na shirika la UN linaloshughulikia masuala ya wanawake.
Bara la Afrika linaongoza kwa mauaji ya wanawake na wasichana
Kulingana na data za Umoja huo, mauaji dhidi ya wanawake yameongezeka katika maeneo mengi ya bara la Afrika, lililokuwa na idadi kubwa ya ukatili huo dhidi ya wanawake na wasichana mwaka 2024 iliyofikia 22,600. Bara la Asia lilifuata likiwa na mauaji 17,400, Marekani 7,700, Ulaya nayo visa hivyo vikichangia wanawake na wasicha 2,100 kuuwawa huku eneo la Pasifiki mauaji hayo yakifikia 300 kwa mwaka huo wa 2024.
Afrika imekuwa na idadi hiyo kubwa ya mauaji ambako waathirika na wanaofanya matendo hayo walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi au mtu wa karibu sana wa familia. Inakadiriwa wanawake au wasichana watatu kati ya 100,000 ndio wanaokumbwa na matukio hayo. Barani Ulaya visa hivyo vilishushwa hadi asilimia 0.5.
Mwaka 2003 takriban wasichana 51,000 na wanawake duniani waliuwawa na watu wa familia zao au wapenzi wao ikilinganishwa na wanawake na wasichana 85,000 waliouwawa kutokana na uhalifu dhidi ya wanawake.