#HABARI: Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) limetangaza mafanikio makubwa katika msimu wa minada ya Korosho baada ya kuuza jumla ya tani 273,000 za Korosho ghafi kupitia minada 17, ambapo thamani ya mauzo hayo imefikia shilingi Bilioni 871 ambazo zote tayari zimelipwa kwa wakulima.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka TMX Prince Philemon Mng’ong’o, amesema fedha hizo zimepelekwa moja kwa moja katika vyama vikuu vya ushirika vinavyokusanya Korosho kutoka kwa wakulima katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Ruvuma.

Mng’ong’o amesema mfumo wa TMX umeendelea kuleta ufanisi mkubwa katika uuzaji wa mazao ya wakulima hususan Korosho kwa kuhakikisha uwazi ushindani wa bei na ulipaji wa haraka kwa wakulima.

Hatua hiyo inaendelea kuimarisha imani ya wakulima kwa mfumo wa TMX na kuongeza ushindani wa kampuni za ununuzi, hali inayochochea bei bora kwa wakulima.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *