#HABARI: Serikali imeendelea kuanzisha Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi, kuanzia ngazi ya Vijiji/Mtaa, Kata, Wilaya na Mkoa ambapo katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025, jumla ya Majukwaa 15,147 yameanzishwa, ambayo yameleta chachu kwa wanawake ya kujifunza masuala ya ujasiriamali, elimu ya fedha na uwekezaji.
Hayo yamesemwa na Naibu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Mary Prisca Mahundi, wakati akizungumza na wanavikundi vya malezi na matunzo ya watoto Kata ya Ihumwa jijini Dodoma.
Mahundi amesema katika eneo la fursa za kiuchumi, Wizara inaratibu na kusimamia jukumu la kuwezesha kiuchumi wafanyabiashara ndogondogo na wao wakiwa miongoni mwao watatambuliwa na kuwasajili na kutoa mikopo yenye masharti nafuu, katika zoezi linalosimamiwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa TEHAMA pamoja na Maafisa Biashara ngazi ya Mikoa na Halmashauri.
“Tangu zoezi hili lilipoanza mwezi Februari, 2024 hadi kufikia tarehe 26 Novemba, 2025 jumla ya wafanyabiashara ndogondogo 115,035 (Ke 70,894: Me 44,141) wamesajiliwa na jumla ya wafanyabiashara ndogondogo 44,336 waliosajiliwa wamelipia vitambulisho vyao na kwa kutumia vitambulisho hivyo, Benki ya NMB imetoa mikopo ya kiasi cha Shilingi Bilioni 9.8 z kwa wafanyabishara hao”amesema Naibu Waziri Maryprisca.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.