
Mkutano wa pili wa Umoja wa Afrika wa mabadiliko ya hali ya hewa, unaanza rasmi hii leo jijini Addis Ababa nchini Ethiopia mkutano huo ukinuia kuleta maono ya pamoja kukabiliana na changamoto za kimzingira na jinsi ya kufadhili miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya hewa barani Afrika .
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakuu wa nchi na serikali zaidia ya 40 wanahudhuria mkutano huo pamoja na wanaharakati zaidi ya 25,000 wa mazingira na watunga sera pamoja na wadau wengine.
Mkutano huu unafanyika wakati huu, mabadiliko ya tabia nchi yakiendelea kusababisha madhara makubwa ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.
Majanga kama mafuriko na uakme ni miongoni mwa mambo ambayo ni athari kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha, changamoto ya tetemeko la ardhi linaendelea kuwa athari nyingine, ya mabadiliko ya tabia nchi.
Nchi tajiri zinazoongoza kwenye uchafuzi wa hali ya hewa, zilizoahidi kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutoa ahadi ya Mabilioni ya Dola, bado hazijatejeleza ahadi hiyo.