Baadhi ya wazee katika kijiji cha Nyijundu, Wilaya ya Nyang’hwale, mkoani Geita wamejitokeza leo Disemba mosi 2025 kupima maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani na kujenga uelewa wa kupima afya mara kwa mara.
Wakizungumza na mwandishi wa #AzamTV mkoani humo, wazee hao wamesema kilichowasukuma kujitokeza ni kutokana na jukumu kubwa walilonalo la kusimamia familia zao, ambapo wamekua wakiwahudumia wagonjwa nyumbani, hivyo ni vyema wafahamu hali ya afya zao.
#Azamtvupdates
Mhariri | @abuuyusuftz