
Israel imefahamisha hivi leo kwamba itafungua kivuko cha Rafah katika kipindi cha siku chache zijazo, kuwaruhusu Wapalestina kutoka Gaza kuingia Misri.
Netanyahu aomba kupatiwa msamaha wa Rais
Jeshi la Israel kupitia kitengo chake kinachosimamia majukumu ya kuratibu shughuli za kutoa msaada Gaza,COGAT, limetowa taarifa hiyo bila ya kufafanuwa ikiwa yatakuweko masharti ya kuamuwa nani anaruhusiwa kuondoka Gaza.
Israel pia imesema hivi leo, kwamba matokeo ya uchunguzi wa mabaki yaliyorudishwa kutoka Gaza sio ya mateka wake waliochukuliwa na Hamas kufuatia shambulio la Oktoba saba,2023.
Kundi la Hamas bado halijatowa tamko kuhusu taarifa hiyo ya Israel ambayo inaweza kusababisha changamoto katika makubaliano tete ya usitishaji vita.