#HABARI: Mwezi Novemba, 2025 Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imefanya Operesheni mbalimbali zilizofanikisha ukamataji wa jumla ya kilogramu 3,799.22 za Dawa za Kulevya, kuteketeza Ekari 18 za Mashamba ya Bangi pamoja na kutaifisha mali za wahalifu wa Dawa za Kulevya zenye thamani ya shilingi Bilioni tatu na milioni mia tatu na nne (3,304,000,000/=), watuhumiwa 84 walikamatwa kuhusiana na dawa hizo.

Katika kuendeleza hatua za kukabiliana na uhalifu wa Dawa za Kulevya, Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, ilitoa maamuzi ya kutaifishwa kwa mali zenye thamani ya Bilioni Tatu na milioni mia tatu na nne (3,304,000,000/=) za watuhumiwa Saleh Khamis Basleman na Gawar Bachi Fakir, ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kujihusisha na Biashara ya Dawa za Kulevya, mali hizo zinajumuisha nyumba, viwanja na magari.

Maombi ya kutaifishwa kwa mali hizo yaliwasilishwa Mahakamani hapo kufuatia uchunguzi uliofanyika na ikabainika kwamba, watuhumiwa hao wanamiliki mali ambazo zilipatikana kwa njia za uhalifu wa Biashara ya Dawa za Kulevya.

Utaifishaji wa mali hizo umefanyika chini ya Sheria ya Mazao ya Uhalifu Sura ya 256 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Sura ya 200 na Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Namba 5 ya mwaka 2015.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *