#HABARI: Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amejipanga kuanza ziara maalum ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kata 142 za Mkoa huo, ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za serikali kwa lengo la kutatua changamoto za wananchi.

Akizungumza na wanahabari Mkuu huyo wa Mkoa, amesema kuwa ziara hiyo itafanyika chini ya kampeni maalum iitwayo ‘Tunavua buti ama hatuvui, tukutane saiti’, ambayo ni muendelezo wa kampeni ya awali ya ‘Sivui buti mpaka kieleweke’

Kampeni hiyo itakayoanza kuanzia Desemba 4, 2025, inalenga kukagua miradi katika sekta mbalimbali, kusikiliza na kutatua kero za wananchi, pamoja na kutoa maelekezo kwa watendaji kuhusu utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo yote ya umma na taasisi binafsi.

Sendiga amesema kupitia ziara hiyo, serikali inakusudia kuimarisha uhusiano kati ya wananchi na viongozi wao, kukuza ushirikiano baina ya watendaji na wananchi wanaohudumiwa, pamoja na kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za miradi ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha inaonekana.

Amebainisha kuwa ziara hiyo itafanyika katika kata zote 142 za Mkoa wa Manyara, na kusisitiza kuwa hakuna mradi au changamoto ya wananchi itakayopuuzwa huku akiwataka watendaji wa serikali na wa kata kuhakikisha taarifa zao zinakamilika na zinawasilishwa ipasavyo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *