Baadhi ya wakulima wa pamba mkoani Simiyu wamekiri kupata hasara katika msimu uliopita wa kilimo kutokanana kukosa elimu sahihi ya matumizi ya mbolea sambamba na kufanya kilimo cha kienyeji.
Wakulima hao wamekiri hayo walipotembelewa na wataalamu wa kilimo wa Wizara ya Kilimo wanaotekeleza mradi wa utoaji wa ruzuku ya pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea na mbegu bora za mahindi.
Joyce Mwakalinga amezungumza na wakulima hao sambamba na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha kufahamu kiundani hali hiyo sambamba na mpango wa maandalizi kuelekea msimu wa kilimo kwa mwaka 2025/2026.
Simiyu, Mara, Mwanza, Geita pamoja na Kagera ni mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa pamba nchini.
Mhariri @moseskwindi