
Rais wa zamani Jair Bolsonaro, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 27 jela kwa jaribio la mapinduzi, amemuidhinisha mwanawe mkubwa, Flavio, kuwakilisha kambi ya wahafidhina katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 2026.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Ni kwa hisia kubwa ya uwajibikaji kwamba ninathibitisha uamuzi wa kiongozi mkuu wa kisiasa na maadili wa Brazil, Jair Bolsonaro, kuniamini katika dhamira ya kutekeleza mradi wetu kwa taifa,” ameandika Flavio Bolsonaro, seneta mwenye umri wa miaka 44, kwenye mtandao wa kijamii X siku ya Ijumaa, Desemba 5, 2025.
Ugombea wake umethibitishwa muda mfupi baadaye na Valdemar Costa Neto, rais wa Chama cha Liberal (PL), chama chake cha kisiasa, katika taarifa: “Flavio Bolsonaro ni jina lililoteuliwa na Jair Bolsonaro kuwakilisha chama katika uchaguzi wa rais,” amesema.
Tangazo hili linafungua njia ya ushindani na rais wa sasa wa mrengo wa kushoto, Luiz Inácio Lula da Silva, mwaka ujao.
Luiz Inácio Lula da Silva, ambaye ana umri wa miaka 80, alitangaza mnamo Oktoba kwamba angeomba muhula wa nne, baada ya kipindi chake cha kwanza kama rais kuanzia 2003 hadi 2010. Kisha akabadili kauli yake wiki hii, akitangaza kwamba “labda angekuwa mgombea” wa urais katika ujachuzi ujao.
“Sitasimama tu na kutazama demokrasia yetu ikiporomoka (…) Ninajiweka mbele ya Mungu na mbele ya Brazil ili kutimiza dhamira hii,” ameongeza Seneta Bolsonaro.
Tangazo hili linakuja huku kukiwa na sintofahamu katika nchi hii kubwa zaidi ya Amerika Kusini kuhusu ni nani angewakilisha kambi ya wahafidhina katika uchaguzi wa 2026, kutokana na kutokuwepo kwa Jair Bolsonaro, ambaye anazuliwa tangu mwishoni mwa mwezi Novemba na kwa hivyo hastahiki.
Gavana wa jimbo la São Paulo, Tarcisio de Freitas, na mke wa Rais wa zamani Michelle Bolsonaro pia walikuwa wanatazamiwa kuwa wagombea.
Udugu wa Kisiasa
“Flávio Bolsonaro ni mwanasiasa mwenye usawa, uzoefu, aliye wazi kwa mazungumzo. Kazi yake inaonyesha ukomavu, uwajibikaji, na maono ya busara ya changamoto za Brazil,” Luciano Zucco, mbunge wa Chama cha Liberal, ameliambia shirika la habari la AFP.
Ingawa anachukuliwa kuwa wa wastani zaidi kuliko ndugu zake wengine watatu ambao wamefuata siasa, mtoto mkubwa wa Jair Bolsonaro pia amezua utata.
Mnamo mwezi Oktoba, kwa mfano, alipendekeza kwamba Marekani ishambulie boti huko Rio de Janeiro ili kupambana na biashara ya dawa za kulevya, kama ililivyofanya nje ya pwani ya Venezuela.
Kaka yake mdogo, Eduardo Bolsonaro, mbunge, amekuwa akiishi Marekani kwa miezi kadhaa, ambapo anashawishi utawala wa Trump kuingilia kati kwa niaba ya baba yake.
Watoto wengine wawili wa rais huyo wa zamani, Carlos na Jair Renan, ni madiwani wa jiji huko Rio de Janeiro (kusini-mashariki) na Balneario Camboriu, mtawalia.
“Seneta Flavio Bolsonaro, mtoto mkubwa wa Jair Bolsonaro, atakuwa mgombea wa urais mnamo mwezi Oktoba 2026,” Eduardo Bolsonaro ametangaza katika ujumbe kwa Kiingereza kwenye mtandao wa kijamii wa X.
© 2025 AFP