
Katika Taarifa yake Msemaji wa Polisi nchini humo David Misime amesema maafisa wameona miito ya kufanyika maandamano katika mitandao ya kijamii lakini akasisitiza kuwa hadi sasa hakuna hata mtu mmoja aliyetoa taarifa rasmi kwa polisi kuhusu kufanyika maandamano hayo. Haya yanajiri wakati matukio yanayoendelea Tanzania yakisababisha Marekani kusema inatathimini upya mahusiano yake na Tanzania kufuatia kile ilichosema ni kubinya uhuru wa watu kujieleza na uhuru wa kidini. Uchaguzi wa Oktoba 29 uliomrejesha madarakani rais Samia Suluhu Hassan aliyetangazwa kupata asilimia 98 ya kura, ulikumbwa na vurugu huku upinzani na mashirika ya binaadamu yakisema zaidi ya watu 1000 waliuwawa.