Katibu Msaidizi wa idara ya Mabinti na Uwezeshaji wa Taasisi ya Mama Asemewe Bi. Beatrice Mwahegili amewataka Vijana hususani Mabinti wa Kitanzania kuheshimu, kulinda na kuitunza amani ya Tanzania, akisisitiza kuwa hakuna Tanzania nyingine zaidi ya hii ya sasa na ni gharama kubwa kurejesha amani pale itakapopotea.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dodoma leo Alhamisi Disemba 04, 2025, amewataka Vijana kuamka na kutokubali kutumika kwa maslahi ya watu wachache, akiwataka pia kuwakataa wale wote wanaohamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani nchini.