Mkuu wa Mkoa wa manyara Queen Sendiga anatarajia kuanza ziara y kampeni maalum iliyobeba jina la Sivui buti hadi kieleweke Dec 4 ambayo inalenga kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali na kufanya mikutano ya wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Sendiga amesema pamoja na wataalam kupaswa kuwepo maeneo ya miradi inakotekelezwa na taarifa za miradi lakini wananchi watashirikishwa kuweza kueleza juu ya miradi hiyo ambayo inatakelezwa kwao.
Aidha sendiga amebainisha kuwa kampeni hiyo ilianza mapema April mwaka huu kwa kutembelea Kata mbalimbali na kuonyesha mafanikio ya kuongeza uwajibikaji kwa watumishi.