Nyerere katika ujamaa wake na falsafa ya kikomunia au kikomunist aliweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa warusi na wachina , na Mrekani aliijua nguvu ya nyerere na Tanzania
ambaye alikuwa na ushawishi wa hali ya juu sana, Kila walipofikilia kuja africa walimfikiria mwalimu Nyerere atakavyowashawishi wengine kukataa hoja zao hivyo ilikuwa muhimu kwa Marekani kuzungumza na Nyerere
Basi mwaka 1964 Rais wa Marekani aliona ni vema kukutana na mwalimu Nyerere
kuzungumzia suala ili la jinsi gani amerika awekeze afrika na kuweza kutimiza maelngo yao, lakini Nyerere aliwakatalia akasema kwamba haitawezekana yeye kuweza kukubali ubepali na ukoloni mamboleo
Sasa Urusi baada ya kusikia hivyo wakakamata fursa kwa kutoa nafasi kwa watanzania kujifunza nchini kwao ujamaa na wengine kujifunza udaktari hata ujasusi pia nadhani hayati luis shika angekuwepo angenielewa zaidi hapa
lengo la Urusi kufanya hivyo likiwa kuwashawish zaidi Tanzania kuwa upande wa USSR kuliko USA, baada ya mwalimu Nyerere kujua kwamba kumbe Tanzania ni muhimu akawachezesha ngoma kwamba Tanzania afungamani na upande wowote
Tangu siku hiyo sera ya Tanzania kutofungamana na upande wowote inadumu hadi leo pia tangu siku hiyo mapambano ya ushawishi ya Marekani na Urusi yalianza rasmi Tanzania, ambapo Marekani aliwekeza kijamii huku Urusi akiwekeza kiusalama zaidi
MATEJOO