#HABARI: Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso, amewaomba wanawake wote nchini wawe mstari wa mbele katika kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili aweze kufanikisha azma yake ya kuwaachia wananchi tabasamu mwishoni mwa uongozi wake.
Paresso alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) lililofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
Katika baraza hilo, aliahidi kushirikiana kwa karibu na wabunge wenzake wa Viti Maalumu mkoa wa Arusha, Chiku Issa na Marirta Gido, katika kutekeleza majukumu yao ya kibunge. Lengo lingine ni kujenga chama pamoja na jumuiya zake ili kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kustawi na kuimarika zaidi.
“Namshukuru Mwenyekiti wa UWT kwa mwaliko huu ambao ni wa kwanza tangu nimekuwa Mbunge baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2025, nipo tayari kujifunza kwenu, nitakua tayari kuelekezwa na kuonywa,” alisema Paresso, akionyesha utayari wake wa kufanya kazi na jumuiya hiyo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania