Hiki ni kikosi cha tano cha polisi wa Kenya kufika huko Haiti kisiwa kilichokumbwa na ghasia tangu kuanza kuhudumu kwa misheni ya polisi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Kenya ina polisi zaidi ya 700 nchini humo.

Kikosi kikosi hiki tajwa cha  maafisa wa polisi kutoka Kenya kinaungana na polisi wengine zaidi ya 700 wa nchi hiyo ambao tayari wanafanya kazi pamoja na Polisi ya Haiti kama sehemu ya kikosi cha kimataifa kilichoimarishwa kwa wanajeshi na polisi kutoka Jamaica, Guatemala na El Salvador.

“Hadi sasa tumetekeleza vyema oparesheni na kutoa vipigo vikali kwa magenge yanayolitesa taifa hilo”, amesema Kamanda wa Kikosi cha Kukabiliana na Magenge ya Uhalifu Godfrey Otunge wakati akiwasalimu polisi  wapya wa Kenya katika uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa wa Haiti.

Baraza la rais la mpito la Haiti lilipitisha sheria ya uchaguzi wiki iliyopita ya kuendesha nchini uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban muongo mmoja, na kuiruhusu serikali  kuchapisha kalenda rasmi ya uchaguzi iliyosubiriwa kwa muda mrefu na wananchi.

Sheria hiyo ya uchaguzi imepitishwa huko Haiti huku baadhi ya wajumbe wa baraza la rais la mpito wakishinikiza kuondolewa madarakani  Waziri Mkuu Alix Didier Fils-Aimé, akiwemo Fritz Alphonse Jean, ambaye hivi karibuni aliwekewa vikwazo na serikali ya Marekani. Fritz Alphonse alikuwa mwenyekiti wa tatu wa baraza la rais la mpito  la Haiti ambaye alihudumu kuanzia mwezi Machi hadi Agosti mwaka huu. 

Godfrey Otunge Kamanda wa Kikosi cha Kukabiliana na Magenge ya Uhalifu ametuma ujumbe wa matumaini kwa wananchi wa Haiti akisema kuwa “Hatutapumzika hadi lengo letu la pamoja litimie: Tutakabiliana na magenge ya uhalifu hadi Haiti iwe salama, iendeshe uchaguzi huru na wa haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *