Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya hali ya usalama nchini kwa kipindi cha saa sita tangu lilipotoa taarifa ya awali majira ya saa 6 mchana leo tarehe 9.12.2025.
Hali ya usalama nchini ni shwari na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimeendelea kuimarisha usalama wa taifa letu, maisha na mali za wananchi hadi muda huu wa jioni.
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama vingependa kuwahakikishia kuwa, kuanzia majira haya ya jioni vitaimarisha zaidi ulinzi na usalama tunapoelekea usiku ili kuzuia na kudhiti vitendo vyovyote vinavyoweza kuwa ni tishio la kiusalama.
Aidha, Jeshi la Polisi lingependa kutoa wito kwa kila mmoja wetu kuendelea kuzingatia kanuni za kiusalama na kuendelea kutii sheria kwani kila mmoja anahitaji kuwa salama wakati wote.
Cc: Imetolewa na;
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma,Tanzania