Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza limeahidi kuendelea kusimamia shughuli za maendeleo na kuongeza mapato ya halmashauri hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Yanga Makaga, mara baada ya kuchaguliwa tena na baraza hilo, ikiwa ni awamu yake ya tatu kutumikia nafasi hiyo.

Makaga amesema baraza hilo litaweka mkazo katika kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato, ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga, amewapongeza madiwani kwa kuaminiwa na wananchi, na kuwataka kufanya kazi kwa kuweka mbele maslahi ya wananchi wanaowawakilisha.

Katika baraza hilo, jumla ya madiwani 35 wamekula kiapo cha kuwatumikia wananchi, sambamba na kufanya uchaguzi uliopelekea Yanga Makaga kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri, huku Fortunatus Nzwagi
akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.

Aidha, baraza hilo limeunda pia kamati mbalimbali za halmashauri kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa majukumu ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Taarifa ya mkurungezi wa halmashauri hiyo Binuru Shekidele imeonyesha kasi ya ukusanyaji wa mapato.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *