#HABARi: Jeshi la Polisi lingependa kuwajulisha kuwa, hadi muda huu wa mchana tarehe 9/12/2025 hali ya usalama wa nchi ni shwari.

Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuimarisha usalama nchini sambamba na kulinda maisha ya watu na mali zao aidha, Jeshi la Polisi lingependa kutoa wito kwa wananchi picha zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kuna maandamano yameanza.

Taarifa hizo siyo sahihi ni za matukio ya nyuma yakiwepo ya terehe 29, 30, 31 mwezi wa 10, 2025. Zingine ni za nyuma zaidi mfano, moja ni tukio la mwezi Juni 2025 ambapo kabila la wamaasai walikuwa na sherehe za jando walizofanyia msitu wa TANAPA Jijini Arusha.

Ikumbukwe kuwa, maandamano yanayopewa jina la
maandamano ya amani yalipigwa marufuku toka tarehe 5 Disemba 2025 kwani hayakidhi matakwa ya kisheria ikiwepo sheria mama yaani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Polisi na Polisi
Wasaidizi sura ya 322.

Aidha, tunatoa wito kwa wananchi waendelee kufuata sharia kwa manufaa yetu sote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *