
Rais wa zamani wa Iraq Barham Saleh, kutoka jamii ya Wakurdi, ameteuliwa kuwa mkuu wa UNHCR, Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, chanzo cha Umoja wa Mataifa, kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, kimesema leo Ijumaa, Desemba 12.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Atamrithi Mtaliano Filippo Grandi mwezi Januari, ambaye alitumia miaka kumi kama mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lonalohudumia Wakimbizi (UNHCR). Wagombea wengine wengi pia walikuwa wamewasilishwa, akiwemo Meya wa Paris Anne Hidalgo na Jesper Brodin, Mkurugenzi Mtendaji anayeondoka wa kampuniinayomiliki maduka mengi ya Ikea.
Bw. Saleh, 65, atachukua madaraka huku UNHCR ikikabiliwa na mgogoro mkubwa: idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao duniani kote imeongezeka mara mbili katika miaka kumi, lakini ufadhili wa misaada ya kimataifa unapungua sana, hasa baada ya kurejea kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House mwaka huu.
Shirika hilo pia limelazimika kupunguza zaidi ya robo ya wafanyakazi wake tangu mwanzo wa mwaka, karibu wafanyakazi 5,000.
Barham Saleh, ambaye alisomea Uingereza, anachukuliwa kuwa mwanasiasa wa mwenye msimamo wa wastani. Alikuwa mwanachama wa mamlaka ya mpito iliyoanzishwa na amri ya kijeshi ya Marekani baada ya kupinduliwa kwa utawala wa Saddam Hussein kufuatia mashambulizi yaliyoongozwa na Marekani mwaka wa 2003.
Kisha alihudumu kama Waziri wa Mipango katika serikali ya shirikisho iliyoundwa baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Iraq mwaka wa 2005. Mwaka mmoja baadaye, akawa Naibu Waziri Mkuu chini ya Nouri al-Maliki, na baada ya muhula wake kuisha, alirudi Erbil mwaka wa 2009 kuhudumu kama mkuu wa serikali ya Mkoa wa Kurdistan hadi 2011.
Akiwa mtoto wa jaji na mwanaharakati wa haki za wanawake, Barham Saleh aliongoza Iraq kuanzia mwaka 2018 hadi 2022, nafasi ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa imehifadhiwa kimya kimya kwa Mkurdi tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka wa 2005.
Mnamo mwaak 2014, baadhi walitabiri kurudi kwake Baghdad, wakati huu akiwa katika nafasi ya Rais wa Jamhuri, lakini dakika za mwisho, Saleh alijiondoa na kumpendelea Fouad Massoum, ambaye pia ni mwanachama wa chama chake, Muungano wa PUK.
Mzaliwa huyu wa Sulaimaniyah, ngome ya PUK, pia aliongoza miradi mikubwa katika jiji hili la pili kwa ukubwa huko Kurdistan, hasa akitetea kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Marekani cha Sulaimaniyah.