
Mkuu wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa ameonya leo Ijumaa Desemba 12, 2025, kuhusu tishio la “vurugu za kikanda” katika eneo la Maziwa Makuu, kufuatia shambulio jipya la kundi la kisiasa na kijeshi la AFC/M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Katika siku za hivi karibuni, shambulio jipya lililoanzishwa na AFC/M23 huko Kivu Kusini limefufua kielelezo cha kutokea kwa mgogoro mpya wa kikanda wenye athari zisizohesabika,” Jean-Pierre Lacroix ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, pia akielezea wasiwasi kuhusu “kugawanyika” kwa DRC.
Siku ya Jumatano, mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa eneo la Maziwa Makuu alitoa picha ya kutisha mbele ya Baraza la Usalama kuhusu hali mashariki mwa DRC, iliyoonyeshwa na mvutano unaoendelea kati ya nchi hiyo na Rwanda, na hatari ya vurugu kuikumba kanda nzima.
Katikati mwa wiki hii Kundi la waasi wa M23 walichukuwa udhibiti wa mji wa Uvira, mkoani Kivu Kusini, mashariki mwa DRC bila upinzani wowote, baada ya kuyateka maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na Kiliba, Sange, Luberizi, Lubarika, Bwegera, Luvungi na Katogota baada ya mapigano mali na jeshi la DRC (FARDC) na washirika wake Wazalendo na wanajeshi wa Burundi.