Mbunge pekee wa viti maalumu mkoa wa njombe kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Sigrada Mligo, amewaomba viongozi wa serikali na viongozi wa siasa, washirikiane katika kuujenga mkoa huo ili kuwaletea wananchi maendeleo pasi kujali tofauti zao kisiasa.
Sigrada ametoa kauli hiyo katika kikao kazi cha viongozi wa serikali za mitaa mkoa wa njombe kilicho itishwa na mkuu wa mkoa Anthony mtaka ili kuwajengea uwezo watumishi katika jwanda wa sheria na mipaka ya kiutawala.
Sigrada amenukuliwa akisema, “Mimi nimeteuliwa na Tume na sio chama changu cha siasa. Kwahiyomimi ni mbunge wa mkoa mzima na tanzania na niko tayari kusikiliza maoni na ushauri wenu katika dhima ya kunijenga ili tushirikiane kuiletea maendelea Njombe”. Alisema Sigrada Mligo mbunge vitimaalumu mkoa wa njombe kupitia CHAUMA.
Miongoni mw amaeneo ya msingi aliyoyagusia ni pamoja na chanzo cha migogoro ya ardhi, akitaja sababu kadhaa ikiwemo uchache wa makamishna wa viapo katika kusimamia kesi za ardhi, mabaraza ya ardhi kupewa mamlaka ya kufanya maamuzi kinyume na sheria ya ardhi nyumba na makazi, pamoja na baadhi ya wanasiasa kwa kushirikiana na wenyeviti wa vijiji kufanya maamuzi ya umilikishaji ardhi bila kuzingatia sheria na taratibu za umiliki ardhi.
Mwandishi @dkhan1410
@RFAOnline
@HabaroStartv