Wakati kukiwa na kilio cha wananchi kuhusu upatikanaji wa maji katika baadhi ya maeneo nchini, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekiri kukabiliwa na upungufu mkubwa wa uzalishaji katika maeneo inayoyahudumia.

DAWASA inasema chanzo cha hali hiyo ni kushuka kwa uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 270 kwa siku hadi milioni 50 kwa sasa, jambo linalosababisha maeneo mengi ya Dar es Salaam na Pwani kukumbwa na uhaba wa maji na hivyo kuhitaji mgao.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *