Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu ameipongeza Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa kusuluhisha migogoro ya kazi 4,339 hadi kufikia Septemba mwaka huu.
Ameihimiza CMA kuendelea kuwekeza katika teknolojia, hususan kuboresha mfumo wa e-Utatuzi, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuongeza ufanisi wa kushughulikia migogoro. Ametaka mazingira rafiki na wezeshi yawepo kwa watumiaji wa mfumo huo, ili kuufanya kuwa nyenzo madhubuti ya kumaliza migogoro kwa wakati.
Awali, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Rahma Kisuo, ameitaka tume hiyo kuweka msisitizo katika usawa na haki mahali pa kazi, sambamba na kuimarisha mbinu za usuluhishi kama njia ya msingi ya kumaliza migogoro ya kikazi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa CMA, Usekelege Mpulla amesema tume itaendelea kuboresha matumizi ya teknolojia ili kuongeza ufanisi katika utatuzi wa migogoro ya kazi, na kuahidi kuendeleza jitihada za kutoa huduma bora kwa wananchi.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi