Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya ajali za barabarani nchini husababishwa na makosa ya kibinadamu ambayo iwapo yatatambuliwa na kuchukuliwa kwa uzito, yanaweza kupunguza ajali hizo kwa kiwango kikubwa.
Mnadhimu wa Polisi, Kitengo cha Usalama Barabarani, SACP Butusyo Mwambelo, amesema hayo wakati wa ukaguzi na utoaji wa elimu ya usalama barabarani mkoani Shinyanga.
#AzamTVUpodates
✍Costa Kasisi
Mhariri | John Mbalamwezi