#HABARI: Bodi ya Bonde la Wami Ruvu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imeendelea kuimarisha tuta la kuzuia maji katika mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu Chini, hatua inayolenga kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

‎Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kupita kwa kipindi cha miezi saba bila kunyesha kwa mvua za Masika katika maeneo mbalimbali nchini, hali iliyosababisha kupungua kwa kina cha maji katika Mto Ruvu.

‎Akizungumza wakati wa kutoa takwimu za hali ya Mto Ruvu, katika mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu uliopo Bagamoyo mkoani Pwani, Mkurugenzi wa Bodi ya Bonde la Wami Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmassi, amesema juhudi zinaendelea kuhakikisha uzalishaji wa maji unaimarishwa licha ya changamoto ya ukame.

‎Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Albert Chalamila, amesema ushirikiano kati ya taasisi hizo utaleta tija na suluhisho la kudumu. Aidha, aliwataka mameneja wote wa DAWASA kuhakikisha maji yanayopatikana yanagawanywa kwa usawa kwa wananchi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *