Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama, umewasili mkoani Ruvuma na kupokelewa na waombolezaji katika Uwanja wa Ndege wa Songea, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas.

Msafara wa waombolezaji ulioufuata mwili huo uliongozwa na Spika wa Bunge, Mussa Zungu, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali.

Baada ya mapokezi, mwili wa marehemu umepelekwa nyumbani kwake katika Mtaa wa Makambi, Manispaa ya Songea, ambako utafanyika sala fupi. Baadaye, mwili huo unatarajiwa kupelekwa katika Kanisa Katoliki la Romani Matogoro kwa ajili ya ibada fupi, kabla ya kurejeshwa nyumbani.

Imeandaliwa na Mawazo Mwaijengo.
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *